Burudani

Model anayedaiwa kutoka kimapenzi na Wema na kudai hamjui Idris Sultan anyoosha maelezo

Model Calisah ambaye anadaiwa kutoka kimapenzi na Wema Sepetu amekataa kuzungumzia mahusiano yake na Wema Sepetu pamoja na kueleza kwanini alisema hamjui aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Wema Sepetu na mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan.
wema-sepetu

Wiki moja iliyopita kupitia kipindi kimoja cha runinga, model huyo alisema hamjui Idris Sultan.

Akiongea na Bongo5 Jumanne hii, Calisah alisema ni kweli kwamba hamjui Idris Sultan na wala hakuongea kwa nia mbaya au kutafuta kiki.

“Mimi nashangaa kwanini watu wamepanic kisa kusema simjui Idris Sultan, kwani yeye ni nani kila mtu amjue?,” aliuliza Model huyo. “Wewe kuna wanamichezo wangapi wameshachukua tuzo kubwa duniani hawajui?. Kwahiyo mimi nadhani watu ambao wananishambulia katika mitandao hawajui nini wanafanya,”

Aliongeza,”Sikusema hivyo kuonyesha dharau, kwa sababu nipo karibu na Wema lakini hajawai kuniambia kuhusu mtu kama huyo na sijawahi kumuona naye, na kama ukiwa na mwanamke halafu akawa azungumzia mwanaume mwingine hizo ni dharau sana. Kwahiyo kiukweli mimi jamaa nimeanza kumjua baada ya watu kinitag picha zake katika mitandao ya kijamii,”

Pia model huyo alisema kwa sasa hawezi kuweka wazi kama ni kweli anatoka kimapenzi na Wema Sepetu huku akidai Wema ndiye atayekuwa na jibu sahihi juu yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents