Michezo

Mohamed Salah hakamatiki EPL, Avunja rekodi ya ‘Torres’ Liverpool

Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya Taifa ya Misri, Mohammed Salah ameonekana kuwa mwiba klabuni hapo baada ya kuendelea kuvunja rekodi na kuweka historia mpya ndani ya klabu hiyo.

Mohamed Salah akifunga goli la kwanza jana dhidi ya Watford

Kwenye mchezo wa jana kati ya Liverpool  na Watford, Mohammed Salah alifunga magoli manne na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 5-0.

Kwa ushindi huo Mohamed Salah kwa sasa ndiye mchezaji anayeongoza kuwa na magoli mengi katika Ligi Kuu Uingereza (EPL), amefunga magoli 28 akiwa amecheza mechi 30 .

Na hizi ni baadhi ya rekodi ambazo amezivunja katika msimu wake wa kwanza tangu ajiunge na klabu ya Liverpool.

-Mchezaji wa kwanza kufunga Hat-trick ndani ya Liverpool tangu kocha wa klabu hiyo, Jürgen Klopp aanze kuifundisha klabu hiyo.

-Mchezaji wa kwanza kujiunga na Liverpool kwenye msimu wa kwanza kufunga magoli mengi kwenye michuano yote (36), rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Fernando Torres magoli (33).

-Mchezaji wa kwanza kutoka Misri kufunga Hat-Trick katika Ligi Kuu Uingereza (EPL).

-Mpaka sasa ndiye mchezaji mwenye magoli mengi kwenye Ligi kubwa tano barani Ulaya (EPL, La Liga, Bundesliga, Serie A na Ligue 1) ambapo anajumla ya magoli 28 akiwa mbele ya Lionel Messi, Ciro Immobile, Edson Cavan na Harry Kane wote wakiwa na magoli 24.

Mpaka sasa Mohammed Salah bado magoli mawili tu ya EPL avunje rekodi inayoshikiliwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba ya kuwa mchezaji wa kwanza Muafrika kufunga magoli mengi kwenye EPL, Drogba alifunga magoli 29 kwa msimu mmoja 2009/10 .

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents