MichezoUncategorized

Mohamed Salah matatani na jeshi la polisi, Liverpool yathibitisha

Klabu ya Liverpool imeripoti kuwa mshambuliaji wake raia wa Misri, Mohamed Salah alishikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kuendesha gari huku anatumia simu.
  Uongozi wa timu hiyo umetoa ripoti hiyo hapo jana siku ya Jumatatu kuwa Salah anashikiliwa na polisi kwakosa la kuendesha gari huku akiwa anachati na simu.

Kipande cha video kimewekwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kinachomuonyesha nyota huyo akiwa anaendesha gari yake aina ya Mercedes huku akichati jambo ambalo ni kosa kwamujibu wa sheria za Uingereza.

Salah ameisaidia timu yake ya Liverpool kuchomoza na ushindi wa mabao 4 – 0 dhidi ya West Ham siku ya Jumapili mchezo uliyopigwa kwenye dimba la Anfield. 

Related Articles

One Comment

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents