Michezo

Mohamed Salah na Roberto Firmino kuikosa Barcelona: Jurgen Klopp akiri ni pigo kwa Liverpool ‘Striker wetu bora kabisa duniani hawatakuwepo’

Kocha Mkuu wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amethibitisha kuwa nyota wake Mohamed Salah ataukosa mchezo wa Champions League dhidi ya Barcelona baada ya kupata majeruhi siku ya Jumamosi.

Jurgen Klopp said in his pre-match press conference that Salah has been ruled out of the tie

Licha ya majeraha hayo Salah aliweza kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-2 mbele ya Newcastle kwenye mchezo wa Primier League.

Kwenye mechi hiyo ya hatua ya nusu fainali ya Champions League itakayopigwa siku ya Jumanne hapo kesho, Liverpool pia itamkosa nyota wake Roberto Firmino.

Kupitia mkutano wake na waandishi wa habari, Klopp amesema kuwa kwa mujibu wa madaktari haruhusiwi kuchza ”Haruhusiwi kucheza, ila anajiskia vizuri lakini hajaimarika.”

”Tunalo tumaini tu, lakini huo ndiyo mpira na hatujakata tamaa kisa kati ya washambuliaji wetu wawili tena bora kabisa duniani hawatakuwepo. hayatakuwa maisha rahisi lakini kwakuwa tupo 11 uwanjani tutajaribu.”

Kwa matokeo hayo Salah atakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Wolves siku ya Jumapili katika mechi ambayo huwenda ikashuhudiwa Liverpool ikishinda taji la Premier League kwa mara ya kwanza baada ya kupita kipindi kirefu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents