Michezo

Mohammed Ibrahim ‘MO’ apeleka msiba kwa familia yake

Kiungo wa klabu ya Simba, Mohamed Ibrahim ‘MO’ amefiwa na mtoto wake mchanga hapo jana siku ya Jumanne katika Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam. Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya timu hiyo zinasema kuwa msiba huo upo nyumbani kwa familia ya mchezaji huyo Mbagala Kiwangwa.

Klabu ya soka ya Simba kupitia katika mtandao wao wa kijamii wa Instagram imetoa pole kwa mchezaji huyo kutokana na msiba mzito uliyomfika.

Klabu ya Simba inatoa pole kwa kiungo wetu@mohammedibrahim04 ‘Mohammed Ibrahim’ kwa kufiwa na mwanae mpendwa, tumeumia sote kwa msiba huu wa mtoto wetu mdogo kabisa.

Klabu ya Simba inatoa pole kwa msiba huu mzito kwako na kwa famila nzima.
Inna lillah wainna ilaihi Raajiun.

TAARIFA: MSIBA WA MTOTO WA MOHAMMED IBRAHIM UPO MBAGALA KIWANGWA

Msiba wa Mtoto wa Mohammed Ibrahim upo nyumbani kwa familia ya Mohammed Ibrahim Mbagara Kiwangwa jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents