Bongo Movie

Monalisa: Umefika muda wa wasanii wa Tanzania kwenda kimataifa

Baada ya mwanadada Lupita Nyong’o wa Kenya kuchua tuzo ya Oscar hapo jana,msanii wa filamu kutoka Bongo, Yvonne Cherry Ngatikwa aka Monalisa amesema huu ndio muda kwa wasanii wa Tanzania na wao kufanya kazi kwa bidii na kuachana na majungu ili kufika kimataifa.

Cdrisa4 (1)

Monalisa alikuwa akizungumza na kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio jana.

“Sisi wenyewe wasanii tuna impact kubwa katika kufanya tusifike kimataifa,kwasababu kama sisi wenyewe hatupendani, majungu yamezidi yaani watu wanavurugiana. Mtu akiwa amefanikiwa kidogo sisi wenyewe hatuwezi kusupport. Kama sasa hivi hiyo issue ya Juma wa Siri ya Mtungi amechaguliwa kuwania tuzo kubwa Nigeria, lakini sioni msanii yeyote kuongelea,sioni msanii yeyote akisema watu wampigie kura ili ashinde kwasababu anaposhinda yeye inashinda Tanzania, inashinda bongo movies, wanashinda wasanii wote wa Tanzania,” alisema Monalisa.

“Lakini hatusapotiani sisi wenyewe. Kwahiyo mimi nadhani tukae now tuamke, tupendane,tufanye kazi yaani tufikirie mbele. Wasanii wengi tunafikiria hapa hapa kwenye bongo movie tu ,tumemaliza basi. Lakini ni muda sasa wa kufanya kazi zenye ubora wa kimataifa kupeleka katika matamasha mbalimbali duniani. Tujitangaze nje hivyo nadhani tutafika kwasababu kama Lupita amepita mtu yoyote anaweza akapita.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents