Burudani

Moni wa Central Zone kuachia albamu mpya

By  | 

Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Morogoro, Moni Central Zone ameweka wazi mpango wake wa kuachia albamu mpya ikiwa ni mwezi mmoja toka atoke kwenye janga la kutekwa na watu wasiojulikana akiwa na Roma Mkatoliki pamoja na watu wengine 2 akiwemo producer wa Tongwe Record.

Moni wa Central Zone

Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Tunaishi Nao’, ameiambia Bongo5 kuwa albamu hiyo tayari imeshakamilika na itaachiwa muda wowote.

“Namshukuru Mungu baada ya matatizo maisha yanaendelea, mtaani tayari nimeachia wimbo wangu mpya ‘Tunaishi Nao’ na unafanya vizuri. Pia kuna albamu yangu mpya inakuja, kila kitu kipo tayari nasubiria tu hali ya hewa ikae poa na mimi niachie yangu,” alisema Moni.

Rapa huyo amedai wimbo wake ‘Tunaishi Nao’ ni wimbo aliouandaa hata kabla ya kupata matatizo ya kutekwa na watu wasiojulika.

Jeshi la polisi bado linaendelea na upelelezi kuhusu tukio hilo.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments