Michezo

Morata kuonesha makali yake kwenye mechi ya Chelsea vs Bayern Munich leo

Klabu ya Chelsea leo itakuwa na kibarua kigumu pale itakapovaana na Mabingwa wa Ligi kuu ya Ujerumani, Bayern Munich mchezo ambao mashabiki wengi wa soka hususani wa Chelsea wanasubiria kumuona mchezaji waliomsajili kwa dau kubwa klabuni hapo msimu huu akitoa Real Madrid, Alvaro Morata .

Morata akiwa mazoezini na kikosi cha Chelsea huko nchini Singapore

Mechi hiyo imekuwa gumzo duniani kote baada ya usajili wa aliyekuwa kiungo wa kati wa Real Madrid, Alvaro Morata kutua klabuni hapo huku vilabu vikubwa kama Manchester United na Bayern Munich.

Tayari kocha wa Chelsea Antonio Conte, amethibitisha kuwa Morata atakuwepo kwenye kikosi kitakacho wakabiri Bayern Munich leo.

Mchezo kati ya Chelsea na Bayern Munich ni mchezo wakuwania kombe la mabingwa mechi za Pre-season na utachezwa huko nchini Singapore kwenye Uwanja wa Taifa majira ya saa 8:00 mchana kwa masaa ya Afrika Mashariki.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents