Michezo

Morocco Yamsifia beki wa Yanga Kiulaya


Kiwango cha hali ya juu alichokionyesha beki wa Yanga, Stephano Mwasika kimemshangaza sana balozi wa Morocco, Tanzania, Abdelilah Benryane.

Balozi huyo alisema kiwango alichonacho Mwasika kinatosha kuwa na sifa na vigezo vyote kulingana na nafasi yake anayocheza kuimudu vizuri.

‘Kati ya wachezaji walionifuraisha ni beki wa kushoto wa Stars (Mwasika) ambaye amecheza vizuri sana, nashangaa kuona anacheza soka Tanzania wakati kiwango chake kinatosha kuchezea ligi za Ulaya.’

Huyu ni beki mwenye uwezo na vigezo na sifa zote za kucheza Ulaya. Anapanda na kushuka,anapiga kros na kukaba kati.Ameonyesha sifa muhimu ambayo beki wa pembeni anatakiwa kua nazo.

‘Pia nimefurahishwa na uwezo wachezaji wa Taifa Stars wanaounyesha,ni timu nzuri naamini baada ya miaka miwili ijayo itakuwa imara zaidi,’ alisema Benrryane

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents