Morocco wabeba kombe la CHAN kwa kishindo mbele ya Nigeria

Michuano ya kombe la Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) imefikia mwisho usiku wa kumkia leo kwa mchezo wa fainali kuchezwa kati ya wenyeji Morocco dhidi ya Nigeria.

Katia mchezo huo ambao ulichezwa katika uwanja wa Stade Mohammed V, Morocco walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Magoli ya Morocco yalifungwa na Zakaria Hadraf ambaye alifunga mabao mawili katika dakika ya 45 na 64. Mengine yalifungwa na Walid El Karti dakika ya 61 na Ayoub El Kaabi aliyefunga dakika ya 73.

Wakati huo huo, kwenye dakika ya 48 katika kipindi cha pili, mchezaji Peter Eneji Moses wa Nigeria alitolewa nje ya uwanja baada ya kupewa kadi ya pili ya njano.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW