Habari

Motorola kuja na simu itakayobashiri unataka kubofya nini na hivyo kuzima apps zisizo muhimu

Moto X ni smarter kuliko smartphone za kawaida. Watengenezaji wa simu za Motorola, wanatarajia kuja na simu za Moto X ambazo zitakuwa na ‘low-power mode’ ambayo itakuwa na uwezo wa kubashiri unachotaka kufanya baadaye na hivyo kuzima apps zisizo muhimu ‘automatically’ ili kutunza chaji.

IMGS7609-X2
CEO wa Motorola, Dennis Woodside

Tangazo la simu hiyo lilitolewa na mwenyekiti mtendaji wa Motorola, Dennis Woodside kwenye mkutano wa D11 huko California.

Motorola imepanga kuzindua simu hiyo baadaye mwaka huu. Moto X itatangenezwa huko Texas na itakuwa ni simu ya kwanza kuzinduliwa tangu kampuni hiyo yenye makao yake jimboni Illinois-tangu inunuliwe na Google mwaka 2011.

Motorola, ilinunuliwa na Google kwa dola bilioni 12.5.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents