Michezo

Mourinho aahidi kutoshangilia wala kuongea chochote endapo timu yake itashinda katika mchezo wa kesho Stamford Bridge

Special one kagoma kutia neno katika mchezo wa kesho

Kocha wa klabu ya Mancheter United na taifa la Ureno Jose Mourinho amefunguka kuhusiana na mchezo wao wa kesho dhidi ya Chelsea ambao utachezewa katika uwanja ambao alikuwa akiutumia kama uwanja wake wa nyumbani kipindi cha miaka minne iliyopita.

Mourinho ameongea hayo wakati akizungumza na Skysport kuhusiana na mchezo wao huo ambao atakutana na Chelsea ikiwa na kochqa mpya ambaye ni Muitaliano Sarri,ikiwa mara ya mwisho akikutana na Muitaliano mwingine ambaye alifukuzwa kwenye klabu hiyo Anthonio Conte.

Mourinho amesema “Ntajikontro mwenye” hayo ameongea baada ya kukumbwa na matukio kadhaa ndani ya wiki iliyopita baada ya kutakiwa kujieleza kuhusiana na kuonekana kutoa maneno machafu baada ya ushindi wake dhidi ya Newcastle.

Mreno huyo aliongeza :- “Kwa mimi ni mchezo kama ilivyo michezo mingine,” alisema Mourinho. “Je, ningependa kushangilia kama ninavyofanya ikiwa timu yangu imepata goli au ushindi katika uwanja wa Stamford Bridge? Sidhani kama itakuwa hivyo.”

“Nadhani nitajaribu kujidhibiti mimi mwenyewe kwa ajili ya kuheshimu uwanja na mashabiki ambao walikuwa upande wangu na uwanja wangu kwa miaka mingi iliyopita, Kwa kufanya hivyo ntakuwa nimepoteza moyo wangu wa kihisia, ambao si rahisi.”

“Nadhani sikuzote natakiwa kufikiria ni wapi nilipo, na ni uwanja gani mimi niko na ambao umati wote umesimama, Mbali na hiyo, ni mechi kama mechi zingine tu kwangu, Mechi ninayotaka kufanya vizuri kwa wachezaji wangu, timu yangu na mashabiki wangu, ndivyo ninavyotaka. ”

alipoulizwa kama aliwajibu FA alijibu “Ndio niliwajibu ila sintoongea chochote”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents