Michezo

Mourinho achanganyikiwa na ‘free-kick’ ya Ashley Young (Video + Picha)

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho ameeleza namna alivyochanganyikiwa na mpira wa adhabu “free-kick” uliyoenda kupigwa na winga wake, Ashley Young katika mchezo wao wa hapo jana usiku dhidi ya Watford.

Mourinho alishtushwa kwa kitendo cha winga huyo kupiga mpira huo uliyokuwa umbali wa mita 30 ilihali si miongoni mwa wachezaji wazuri waliyopangwa kupiga mipira ya haina hiyo.

Wakati wa kwenda kupigwa kwa mpira huo meneja huyo wa United alionekana kuchanganyikiwa kupitia kamera zilizokuwa zikionyesha mchezo huo.

“Nilishitushwa na kitendo cha Paul kumpatia nafasi ile ya kupiga mpira.” Amesema  Mourinho.

“Sikushangazwa na shuti lake bali kupata ile nafasi ya kupiga mpira hakika yupo vizuri na kiwango chake kinaridhisha katika mazoezi kwahio tunafahamu ataendelea kufunga lakini Paul pia amefanya vizuri.”

Wakati huo huo Mourinho ameelezea sababu ya Lukaku kuvalia kiatu cheusi katika mchezo.

Lukaku amevalia kiatu cheusi jana katika mchezo wetu dhidi ya Watford nafikiri anahitaji kupata mdhamini mwingine wa kiatu chake kwakuwa aliyekuwa nae mwanzo wamemaliza mkataba nahiyo ndiyo sababu.”

Katika mchezo wa hapo jana usiku Manchester United imechomoza na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ugenini dhidi ya Watford huku winga ambaye ahkupewa nafasi kubwa ya kufunga Ashley Young akitupia mawili kati ya hayo.

Mourinho haamini kwa kile anachokiona

Meneja huyo wa United anahitaji kuthibitishiwa kwa kile anachokiona ni cha kweli

Bado akionekana kushikwa na butwaa Mourinho

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents