Michezo

Mourinho adai Drogba bado ni miongoni mwa washambuliaji bora duniani

Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho anaamini kuwa mchezaji wa zamani wa Blues, Didier Drogba bado ni miongoni mwa washambuliaji bora duniani.
Drogba-18

Drogba ambaye kwa sasa anaichezea Galatasaray na aliyeondoka Stamford Bridge June 2012, atarejea London kwenye mchezo wa pili wa mabingwa wa Ulaya katika hatua ya 16 dhidi ya Chelsea.

Mshambuliaji huyo wa Ivory Coast alifunga magoli 157 kwenye mechi 342 za miaka nane aliyoichezea Chelsea. Chelsea itakuwa timu ya kwanza ya Uingereza kuingia hatua ya robo fainali kama itaishinda timu hiyo ambayo ni mabingwa wa Uturuki wanaonolewa na kocha wa zamani wa Manchester City, Roberto Mancini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents