Michezo

Mourinho aeleza sababu za kumuweka Pogba benchi dhidi ya Liverpool, asema afurahishwa na Lingard,Mata na Herrera

Kocha wa klabu ya Manchester United Mreno Jose Mourinho amefunguka mengi kufuatia kupoteza mchezo wake dhidi ya Liverpool katika dimba la Anfield siku ya jana katika ligi kuu nchini Uingereza PL.

Mourinho ameongea mengi hasa kwa wachezaji wake hadi kufikia kueleza kwamba wachezaji wa Manchester United hawa viwango vya kutosha vya kuipambanisha na Liverpool.

Mbali nakuongelea hilo lakini pia amemuongelea kiungo wake raia wa Ufaransa Paul Pogba ambaye alianzia benchi katika mchezo wa jana kitu ambacho kiliwafanya watu wapigwe na butwaa kutokana na kiwango cha kiungo huyo ambaye amekuwa kama tegemezi kwa klabu hiyo kubwa.

Nyota huyo wa Ufaransa Pogba alitazama mchezo kutoka kwenye benchi kwa mechi ya pili ya ligi mfululizoza, United ambapo mchezo wa jana ilishindwa kwa goli 3-1.

Kabla ya mchezo Mourinho aliulizwa:- Kiungo ghali zaidi duniani ataanza katika mchezo huu baada ya kumuweka nje katika mchezo uliopita ? Mourinho alijibu “Hapana,” ma kuongeza ” Kwa sababu nina furahishwa na Nemanja Matic, Lingard na Ader Herrera”

Mourinho pia alikuwa ameridhika na Lukaku licha ya mshambuliaji huyo ambaye hakuwa na shuti lolote huku akigusa mpira mara 20 tu, huku akiwa na magoli 6 akiwa kama mshambuliaji tegemezi wa klabu hiyo katika michezo yake 22 msimu huu. Mourinho alisema:- “Nadhani hakuwa na mchezo mbaya kabisa, nadhani alipigana kwa nguvu zote, alikuwa na harakati nzuri,alitengeneza nafasi ya goli pia”

“Wakati mwingine ugusaji wake wa kwanza wa mpira huwa sio mzuri sana na upotezaji wake wa mipira mingi, lakini leo halikutokea. Alikuwa na viungo vyenye uwezo vizuri na alipigana kwa bidii, Kwa kuboresha, alicheza vizuri katika mchezo wa mwisho dhidi ya Fulham na leo ilikuwa mechi ngumu sana kucheza, Nadhani alikuwa mzuri.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents