DStv Inogilee!

Mourinho afunguka kurejea Real Madrid, akunwa na mashabiki wa Los Blancos wanavyotaja jina lake

Jose Mourinho amesema kuwa mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote kati yake na klabu ya Real Madrid juu ya kuwa kocha wa timu hiyo lakini anajiskia fahari kubwa kuona mashabiki wakimtaja jina lake.

Mashabiki hao wa Los Blancos walitaja jina lake kwa kupiga kelele baada ya miamba hiyo ya Hispania kupokea kipigo cha jumla ya mabao 4-1 mbele ya Ajax usiku wa Jumanne.

”Kama walikuwa wanataja jina langu, najivunia kwa hilo lakini Real Madrid wana kocha,” Mourinho ameiyambia El Chiringuito TV nje ya nyumba yake jijini London.

Mourinho ameongeza kuwa ” Bilashaka najivunia, wakati unaskia watu wanaliita jina lako kwa kupiga kelele hakuna cha ziada zaidi ya kufurahi.”

” Sijazungumza na mtu yoyote na kumekuwa tetesi nyingi lakini naamini tetesi katika soka sio nzuri na siyo za kuamini.”

Ingawaje ameonekana kukwepa, lakini Mreno huyo ameripotiwa kurejea tena Santiago Bernabeu.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW