Michezo

Mourinho afunguka usiyoyajua kuhusu Manchester United “Watu wanalaumu wanachokiona hawajui kilichopo nyuma ya pazia”

Aliyekuwa kocha mkuu wa Manchester United ambaye alifukuzwa kazi mwezi wa 12 mwaka 2018, Mreno Jose Mourinho amefunguka mwanzo mwisho kuhusu maisha yote wakati anafanya kazi Manchester United.

Mreno huyo amefunguka yote wakati anaongea na Beln Sports na kusema kuwa “Nadhani kwamba wakati mwingine tunajadili kile tunachokiona, lakini hatujui ni nini kipo nyuma ya pazia Na ndio huathiri kile tunachokiona.

“Nadhani hilo ndio jambo la msingi sana, Ikiwa nawaambieni, kwa mfano, nikiwaambia kwamba moja ya mafanikio mazuri zaidi ya kazi yangu ilikuwa ni kumaliza katika nafasi ya pili na Manchester United katika Ligi Kuu msimu wangu wa Kwanza mnaweza kuamini hicho ?

“Unaweza ukasema ‘mtu huyu anawazimu. Alifanikiwa kushinda mataji 25 na anasema kwamba nafasi ya pili ilikuwa moja ya mafanikio yake bora katika soka akiwa Manchester. Ninaendelea kusema jambo hili kwa sababu watu hawajui kinachoendelea nyuma ya matukio yote haya, Na wakati mwingine sisi, tuliopo upande huu wa kamera, huwa tunachambua mambo kwa mtazamo tofauti zaidi bila kujua vitu kiundani”

Mbali na kuongela hilo Mourinho mara nyingi alikuwa akishutumiwa kwa mtindo wake wa kucheza wa kujihami huko Man United, lakini akawapinga wale ambao wanahoji njia zake za ufundishaji na kusema

“Ni rahisi sana kucheza vizuri na kushindwa kushinda. Ni rahisi sana kuwa nyuma ya wazo la soka fulani bila matokeo,” aliendelea.

“Na watu wanapata matokeo mazuri mara kwa mara – kwa sababu unaweza kushinda pekee na kisha kutoweka – watu ambao wameshinda mara kwa mara wana wazo tofauti kuhusu hilo.”

“Ikiwa unasema kuhusu Guardiola, kuhusu [Carlo] Ancelotti hapo sawa ila vipi kuhusu wale ambapo sio miongoni mwao ambao wanashindi mara kwa mara na kwa muda mrefu, Wako wapi wenye mathara kuhusu matokeo? “

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents