Tupo Nawe

Mourinho akunwa na kitendo cha kipa wa Chelsea kugoma kutolewa ‘Nimependa, alitaka kuonyesha uwezo wake’

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Chelsea na Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa kitendo alichofanya mlindalango wa The Blues, Kepa Arrizabalaga kugoma kutolewa kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Manchester City alikuwa sahihi.

Meneja wa Chelsea, Maurizio Sarri alijikutaka akiingia kwenye sintofahamu dhidi ya golikipa wake, Kepa baada ya kumtaka kutoka nje na kumpisha, Willy Caballero kwaajili ya kuchukua nafasi katika hatua ya mwisho ya mikwaju ya penati.

Akizungumza na DAZN, Mourinho amesema kuwa mlindalango huyo alikuwa sahihi kwakuwa alitaka kuonyesha uwezo wake na alikuwa anajiamini.

“Golikipa alihitaji kuonyesha utu wake, uwezo na kujiamini, alihitaji kuonyesha uwepo wake na kutaka kuiyokoa timu na nimeipenda,” amesema Mourinho.

Mashabiki wa Chelsea wameonyesha kuguswa na mazungumzo ya Mourinho kiasi kumuandikia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakiamini alichosema kilikuwa sahihi na wengine kukinzana na mtazamo wake.

Ikumbukwe kuwa Mourinho aliwahi kutimuliwa ndani ya klabu ya Manchester United kutokana na mahusiano mabaya dhidi ya wachezaji wake.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW