Michezo

Mourinho alipa faini ili kuepuka adhabu ya kwenda jela miezi 12, kwa kosa la kukwepa kodi nchini Uhispania

Kocha wa zamani wa Man United Mreno Jose Mourinho leo tarehe 5 mwezi wa pili 2019 amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela na faini ya euro 182,500 kutokana na kosa la ukwepaji kodi nchini Hispania.

Jose Mourinho alitenda kosa hilo wakati anakinoa kikosi cha Real Madrid na kosa lake linalomkabili ni la haki za mauzo ya picha zake (images), liliotokea mnamo mwaka 2011 na 2012. na kulipa faini ya ziada ya euro milioni 1.98 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 5.2, ili kuepuka adhabu hiyo.

Lakini hatotumikia muda huo wa mwaka mmoja jela baada ya kukubali kosa na badala yake  kubadilishana hukumu kwa faini. Waendesha mashitaka wa Hispania walisema meneja wa zamani wa Manchester United alishindwa kutangaza mapato kutokana na haki za picha katika matangazo ya kodi ya Hispania tangu 2011 na 2012, akiwa kocha wa Real Madrid, "kwa lengo la kupata faida zisizo halali". Habari hizo zinachukua masaa 24 kwa Mourinho ambaye alionekana katika mchezo wa hockey ya barafu huko Urusi Jumatatu jioni.

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents