Michezo

Mourinho amkaribisha Eden Hazard ndani ya United ‘Historia inaonyesha akiwa kwenye kiwango chake Chelsea inakuwa mabingwa 

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa anatamani kumsajili mshambuliaji, Eden Hazard anayekipiga ndani ya Chelsea kwakuwa licha ya kumpenda kwake lakini pia anauwezo wa hali ya juu katika mbio za kuwania ubingwa.

Kwa upande wake Hazard alipokuwa kwenye majukumu ya timu yake ya taifa ya Ubelgiji amewahi kumzungumzia Mourinho ambaye alikuwa naye ndani ya Chelsea na kusema kuwa angependa kufanya naye kazi siku moja.

Wawili hao watakutana hii leo wakati United itakapo shuka darajani Stamford Bridge kuivaa Chelsea lakini Mourinho anaamini atamsajili mchezaji huyo kama ataendelea kusalia Old Trafford.

“Ningelipenda kuwa naye ndani ya Manchester United lakini siamini kama Chelsea watakuja kutuuzia hata hivyo siyo tatizo,”  amesema Mourinho.

Mourinho ameongeza “Historia inaonyesha endapo Eden Hazard anakuwa kwenye kiwango chake kwenye Premier League basi, Chelsea inachukua ubingwa. Hiyo iliwahi kunitokea hata alipokuwa na mimi na hata Antonio Conte.”

“Chelsea imekuwa kwenye nafasi nzuri katika msimamo wa ligi kwa sasa kwasababu yake yeye ni aina ya mchezaji ambaye anaweza kubadili aina yoyote mchezo.”

“Chelsea inaongozwa na watu wenye uzoefu na elimu ya mchezo wa soka ninaamini hawawezi kumuuza Eden na kutua Manchester United. Nafikiri ni kijana mzuri na tunamahusiano mazuri, tulikuwa mabingwa tukiwa pamoja. Kwa mara ya kwanza amekuwa mchezaji bora Premier League akiwa na mimi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents