Michezo

Mourinho anafuraha kuona kikosi chake kimekamilika – Ibrahimovic

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United, Zlatan Ibrahimovic amesema timu hiyo inaweza kuzishinda changamoto zote ambazo inakumbana nazo kipindi hiki katika michuano ya ligi kuu nchini Uingereza na ile ya Klabu bingwa barani Ulaya.

Ibrahimovic, Paul Pogba na Marcos Rojo wamerejea katika kikosi hicho ambacho Jumamosi ya wiki hii iliyopita iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Newcastle United huku ikishika nafasi ya pili nyuma ya jirani zao City wakiachwa kwa alama nane.

Kwa kushinda michezo minne ya hatua ya makundi ya Klabu bingwa msimu huu, United itahitaji pointi moja tu ili kufudhu hatua ya 16 bora ya michuano hiyo huku Jumatano hii ikishuka dimbani kuikabili FC Basle.

Ibrahimovic ameviambia vyombo vya habari vya Uingereza kuwa malengo yao msimu huu ni kuhakikisha wanafanikiwa kuchukua mataji yote mawili la Ligi na Klabu bingwa barani Ulaya.

“Nafikiri kilakitu kinawezekana, tunatimu imara msimu huu tunaamini tunaweza na hilo ndilo lengo letu kushinda mataji.” Amesema Zlatan.

“Nadhani tunaweza kuwapiku City katika nafasi waliyopo sasa, kwani haiwezekani ?. Wiki hii kocha wetu anafuraha kubwa sana kwasababu timu yake imekamilika.”

Ibrahimovic , Rojo na Paul Pogba wamerejea baada ya kutoka kuuguza majeraha kwa muda mrefu huku kiungo wa Ufaransa, Pogba akitupia moja tangu mwezi Septemba.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents