Tupo Nawe

Mourinho apata timu, wachezaji 8 kutua Man United, kocha Everton apewa mechi 3

Jose Mourinho amekataa ofa ya kuifundisha klabu ya Lyon kwa kuwa ameshapata klabu nyengine, hayo ni kwa mujibu wa rais wa ligi ya Ufaransa, Jean-Michel Aulas. (Goal)

Manchester United inajipanga kulipa kitita cha pauni milioni 130 kuwanyakua wachezaji wawili wa Leicester na England; mlinzi Ben Chilwell na kiungo James Maddison, wote wana miaka 22. (Sun)

Hata hivyo kuna ripoti zinadai kuwa klabu ya Chelsea kwa sasa ndio wanapigiwa upatu zaidi kumnasa beki wa kushoto Chilwell pale marufuku dhidi yao ya usajili itakapokwisha. (Mail)Ben Chilwell

Manchester United wanataka kusajili wachezaji wapya nane katika kipindi cha misimu miwili ijayo na tayari wameshaandaa orodha ya wachezaji hao. (Telegraph)

Real Madrid hawataki kupoteza bahati kwa kutomsajili kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, mpaka mwisho wa msimu ambapo kuna uwezekano akaongeza mkataba na klabu yake ya Tottenham. (Marca)

Tottenham pia wana matumaini kuwa watamuuza Eriksen mwezi Januari tili kuzuia wasimpoteze bure mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utakuwa unaisha. (Mirror)Christian Ericsen

Japo rais wa Real Madrid Florentino Perez anataka kumsajili Eriksen, kipaumbele cha kocha Zinedine Zidane bado ni kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 26. (ESPN)

Manchester City wanatafakari juu ya kufanya usajili wa mwezi Januari kwa kumnunua beki wa timu ya Benfica Ruben Dias, 22, ambaye pia anahusishwa na uhamishi kuelekea Manchester United. (Mirror)

Arsenal wapo katika mazungumzo na klabu ya Uturuki Fenerbahce juu ya usajili wa mkopo wa kiungo Mesut Ozil, 30. (Takvim – in Turkish)Mesut Ozil

Kocha wa Everton Marco Silva amepewa michezo mitatu ya kubadili hali ya mambo ama atimuliwe kazi. (Star)

Beki wa Barcelona Gerard Pique, 32, alikaribia kuinunua klabu ya Notts County mwishoni mwa msimu uliopita. (ESPN)

Kocha wa Juventus Maurizio Sarri anataka kumsajili beki wa kushoto Mtaliano Emerson, 25, kutoka Chelsea. (Express)Maurizio Sarri

Arsenal wanamfuatilia kwa karibu kiungo kinda wa klabu ya Feyenoord ya Uholanzi Orkun Kokcu,18, mwenye thamani ya pauni milioni 20. (Mail)

Sampdoria wanakaribia kumteua kocha wa zamani wa Leicester Claudio Ranieri, 67, kama kocha wao mpya. (Tuttosport – in Italian)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa klabu ya Rostov na raia wa Norway Mathias Normann, 23, mwezi Januari. (Goal)

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW