Michezo

Mourinho apewa mechi moja tu ya ligi akipoteza hapo ndio basi tena

Maisha ya Mourinho yapo hatarini

Imeriporipotiwa kuwa kocha wa Manchester United pia raia wa Ureno Jose Mourinho amepewa nafasi ya mwisho ya kuonyesha uwezo katika mchezo dhidi ya Newcastle United na endapo atapoteza katika mchezo huo kibarua chake kitaota nyasi,huku makocha wawili wakidaiwa kurithi mikoba ya Mreno huyo ambao ni Mfaransa Zinedine Zidane pamoja na Muargentina na kocha wa Tottenham Mauricio Pochenttino.

Kocha huo amekuwa na wakati mgumu sana ndani ya klabu hiyo kwani tangu msimu huu uanze 2018/19 ameanza vibaya kwa kucheza michezo 7 akishinda mitatu akipoteza miwili na kupata sare mmoja.

Mbali na kuwa na matokeo mabaya ndani ya klabu hiyo lakini pia amekuwa na mgogoro mkubwa na baadhi ya wachezaji wa timu hiyo,lakini pia akiwa na mzozo na na mkurugenzi wa timu hiyo bwana Ed woodward.

Mzozo huo ulianza pale ambapo timu hiyo haikuweza kusaji mchezaji mzuri na alipoulizwa alimtupia lawama mkurugenzi wa timu hiyo.

Pia mgogoro wake na Pogba unasemekana kuwagawa wachezaji wa timu hiyo wengine wakiwa upande wa Pogba na wengine wakiwa upande wa Mourinho,Pogba alipohojiwa na sky sport aliuponda moja kwa moja mfumo wa kocha huyo na kusema ” Wao wanahitaji kushambulia wakiwa nyumbani ili wapate ushindi ” na alipoulizwa kwanini hawashambulii alisema ” Yeye sio kocha aulizwe kocha”

Lakini baada ya kuhojiwa mchezaji mwingine wa timu hiyo Luke Shaw alisema ” Kocha hana tatizo kwani wao ndio wanaingia uwanjani kucheza na sio kocha kwani kocha kazi yake ni kuelekeza tu nje tatizo liko kwa wachezaji na sio kocha”

Na baada ya hayo yote inasmekana Pogba aliwaambia wachezaji wenzake wakiwa mazoezini kuwa amekatazwa kuongea na vyombo vya habari na uongozi wa timu hiyo.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents