Michezo

Mourinho asema hana mpango wa kuondoka United, akataa kuzungumza na waandishi wa Hispania adai wapo kwaajili ya Madrid 

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa anahitaji kuendelea kuwa mahala hapo na kitu pekee anachofikiria kwa sasa ni kuhusu klabu hiyo.

Mourinho ameyasema hayo hapo jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari kuelekea mchezo wake wa Champions League dhidi ya Juventus utakao pigwa hii leo siku ya Jumanne, baada ya kuulizwa kama angependa kurejea Real Madrid.

”Hapana, maisha yangu yapo hapa, nina mkataba na hadi mwisho wa mkataba wangu ninayo ifikiria ni Manchester United,” amesema Mourinho.

Mkataba wa Mreno huyo unatarajiwa kufikia tamati mnamo mwaka 2020 huku akiwa na chaguo la kuongeza mwaka mwingine. ”Ningependa kusalia hapa hata mkataba wangu utakapo fikia kikomo pia,” amesisitiza Mourinho.

Tayari duru za habari zinasema kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 55, ndiyo chaguo ama pendekezo la mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya klabu ya Real Madrid atakaye kwenda kurithi mikoba ya Julen Lopetegui aliyopo sasa.

”Katika mtazamo wangu, tuna mchezo hapo kesho (leo) na huo ndiyo tunaouangazia na tutakwenda kuukabili kwa gharama zote hivyo hamna ninachofikiria chochote zaidi ya mechi ya kesho.”

Alipoulizwa kuhusiana na Paul Pogba kuelekea mchezo huo dhidi ya timu yake ya zamani ya Juventus, Mourinho amekataa kumzungumzia na hata kuzungumza na waandishi wa habari wa Hispania kwa sababu anaamini kuwa wapo kwaajili ya kuizungumzia Real Madrid na Ronaldo.

” Siupendi huu mkutano, sihitaji kuzungumzia kuhusu Paul Pogba, sihitaji kumzungumzia mtu mmoja mmoja, sihitaji kuzungumza na waandishi wa habari wa Hispania kwasababu wamekuja hapa kwa lengo lao moja tu ni kuhusu Real Madrid na Ronaldo.”

”Kwa sasa nakwenda kucheza na moja kati ya klabu kubwa kabisa duniani, moja kati ya timu kubwa za kiushindani na hicho ndicho kinachonihamasisha mimi na ndicho kilichonileta kwenye mkutano huu lakini huu mkutano unakwenda kwenye muelekeo mwingine, sasa kama unakwenda kwenye muelekeo mwingine na mimi naupeleka kwenye muelekeo mwingine.”

”Cristiano ni mmoja kati ya wachezaji bora kabisa duniani wa muda wote na hakuna mtu yoyote atakaye sema tofauti na hilo, ni mchezaji bora wa muda wote,” amemalizia Mourinho.

Manchester United itashuka dimbani bila kuwepo kwa baadhi ya wachezaji wake kama Marouane Fellaini, Phil Jones, Scott McTominay, Jesse Lingard, Alexis Sanchez na  Diogo Dalot wakati wapenzi wa soka wakimshhuhudia Cristiano Ronaldo akirejea tena Old Trafford lakini akiitumikia Juventus.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents