Burudani ya Michezo Live

Mourinho atema cheche ‘Nishafunga ukurasa na Man United, sitamwacha salama Old Trafford’ 

Kocha mwenye maneno mengi zaidi kunako Premier League, Jose Mourinho amesema kuwa ameshafunga ukurasa na Manchester United hivyo kinachofuata ni kipigo tu ili kuendeleza kuweka rekodi ya kucheza mchezo wake wa nne kwa ushindi pasipo kupoteza akiwa anakisimamia kikosi cha Tottenham.

Tottenham manager Jose Mourinho says his time at Manchester United is 'a closed chapter'

Mourinho anatarajia kukiongoza kikosi cha Tottenham hapo kesho siku ya Jumatano kuwakabili waajiri wake wa zamani Man United kwenye uwanja wa Old Trafford tangu atimuliwe kazi mwezi Desemba mwaka jana.

United imekuwa ikihaha kuhakikisha inarudi kwenye kiwango chake tangu kuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaer, huku ikienda kukabiliana na Spurs inayoshika nafasi ya tano wakitofautiana pointi mbili pekee dhidi ya United waliyopo sehemu tisa.

Mourinho returns to United bidding for his fourth straight win as Tottenham manager

”Kwangu mimi nishafunga ukurasa, niliondoka ndani ya klabu, nikiwa nimetumia muda wangu kuendeleza na kuhakikisha kila kitu kinatokea, nilichukua muda wangu kuhakikisha najiandaa kwa changamoto mpya.” amesema Mourinho.

”Ni ukweli kabisa, United kwangu ipo kwenye kitabu changu cha uzoefu, ipo kwenye kitabu changu cha kumbukumbu.”

Mpaka sasa Tottenham tayari imeshinda michezo yake mitatu ya awali ikiwa chini ya Jose Mourinho, ikitinga hatua ya 16 bora Champions League huku ikifanikiwa kushika nafasi ya tano kwenye Premier League.

Mourinho was sacked by United last December and says he's moved on from what happened

Mourinho ameongeza kuwa ”Kwa sasa siwezi kuwachambua tena United. Kufanya uchambuzi dhidi yao kama wapinzani, jinsi wanavyocheza, tunawezaje kuwafunga, wanawezaji kutufunga kwangu hivyo ndiyo vitu vya msingi ninavyoweza.”

Mreno huyo ameonekana kuvutiwa mno na kurejea kwake katika dimba la Old Trafford ”Najiskia vizuri, napenda kucheza mechi kubwa, napenda kucheza na timu bora na kurudi sehemu ambayo nilikuwa na furaha nayo.”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW