Michezo

Mourinho atembea kwa miguu hadi Old Trafford kuivaa Juventus, apishana na mashabiki njiani bila kumfahamu

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho amesimulia sababu zilizompelekea kutembea kwa miguu hadi katika uwanja wa Old Trafford dakika chache kabla ya kuwavaa Juventus kwenye mchezo wao  wa UEFA Champions League uliyopigwa hapo jana usiku.

Katika kuhakikisha anawahi mkutano wa Champions League dhidi ya Juventus ndani ya dimba la Old Trafford usiku huo, Mreno huyo alilazimika kufanya hivyo ili kuiyepusha United na adhabu ya euro 15,000 ambayo sawa na pauni 13,000 kutoka kwa Uefa kama walivyopata walipochelewa mechi yao na Valencia.

Lakini baada ya kuona basi la timu hiyo limekumbana na foleni kubwa ndipo akalazimika kushuka na kutembea kwa miguu huku akipishana na baadhi ya mashabiki pasipo kumjua akiwa amevalia ‘tracksuit’ za adidas akielekea kwenye dimba la Old Trafford.

“Kama unavyofahamu tulibadili hoteli, hoteli yetu ipo hapo kona tu,” Mourinho ameiyambia BT Sport.

“Wachezaji wamekuwa kwenye basi kwa dakika 45, nilitembea nikiwa na sueta, nimepita katikati ya mashabiki lakini hakuna aliyenifahamu,” amesema Jose Mourinho.

“Imenichukua dakika mbili pekee na nilichofanya kwenye hizo dakika ni kutembea tu wakati wachezaji wakiwa kwenye basi kwa dakika 45.”

“Juventus walikuwa na matatizo kama hayo, nimemfahamisha mwakilishi wa Uefa kuhusiana na hiyo hali kwasababu atuhitaji kuadhibiwa tena.”

United iliwahi kukumbana na foleni wakati ikitokea ‘Lowry Hotel’ na kuelekea Old Trafford wakati wa mchezo wao dhidi ya Valencia Oktoba 2 mwaka huu na Mreno huyo akilalamika kukosa ‘escort’ ya Polisi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents