Michezo

Mourinho atia saini jezi ya Antonio Conte

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho alikuwa anafuraha baada ya kukutwa nje ya hoteli ya Lowry Hotel na wachekeshaji wawili wa Italia siku ya Jumatano huku akionekana na furaha kubwa huenda alifurahishwa na habari za Alexis Sanchez au kuhusu mkataba wake wa kuendelea kuifundisha timu hiyo.

Wachekeshaji hao Alessandro Onnis na Stefano Corti ambao pia ni watangazaji wa kipindi cha runinga cha Italia 1 satirical show, Watangazaji hao walikuwa na nia ya kuzungumza na Mourinho kuhusu msuguano wake na meneja wa Chelsea Antonio Conte.

Conte alikuwa akimuita Mourinho ‘Senile’ na ‘Little Man’ baada mourinho kusema kwamba baadhi ya maneneja wa timu wanatabia kama ‘Clowns’.

Alessandro na Stefano kisha alimuomba Mourinho kutia saini yake katika jezi ya Man United lakini jezi hiyo ilikuwaimeandikwa jina la Antonio Conte na kuckorwa namba moja kwa nyuma. Mourinho aliona ni kitu cha kufurahisha na alicheka kabla ya kuingia ndani ya hoteli hiyo anayoishi.

Na Raheem Rajuu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents