Michezo

Mourinho awatangazia vita waliyopo nafasi za juu EPL, adai United lazima iwendani ya ‘top four’ kabla mwaka 2018 haujaisha 

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amesema kuwa anaamini timu yake itakuwa kwenye moja kati ya nafasi nne za juu kunako msimamo wa ligi kuu England hadi mwishoni mwa mwaka.

United inayoshika nafasi ya nane kwenye msimamo ikiwa na alama 20 inaongozwa na vinara wa ligi Manchester City kwa alama 12 ambao wao mpaka sasa wamejikusanyia jumla ya pointi 32 baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3 – 1 walipokutana .

Kupitia mahojiano yake na waandishi wa habari, Mourinho amesema anaamini atapunguza pengo hili hadi mwishoni mwa mwaka 2018 na kuwa katika moja ya timu nne za juu wakati United ikihitaji pointi saba pekee ili kumfikia Tottenham aliyopo nafasi ya nne akiwa na alama 27.

“Ni pengo kubwa lakini nafahamu hadi ifikapo mwishoni mwa mwezi Desemba tutakuwa na michezo nane ya kuchea, kama sijakosea ipo nane. Tunazungumzia jumla ya pointi 24 hapo ambazo tunazo na ni kuzipigania hivyo naamini tutakuwa kwenye nafasi hizo za juu,” amesema Mourinho.

Man United itashuka dimbani kuikabili timu ya Crystal Palace leo siku ya Jumamosi na Mourinho amethibitisha kuwa Anthony Martial na Marouane Fellaini watakuwa sehemu ya mchezo baada ya kuwa nje kwaajili ya kuimarisha afya zao kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents