Aisee DSTV!

Mourinho awatupia lawama wachezaji wake matokeo ya 2-2 dhidi ya Arsenal

Kocha Jose Mourinho amewalaumu wachezaji wake kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga jambo ambalo limesababisha timu hiyo kupata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Arsenal jana Jumatano usiku.

Matokeo hayo yameiweka Manchester United kwenye ushindani kuwapo kwenye timu nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Makosa ya David de Gea na Marcos Rojo yaliigharimu timu yao jambo ambalo limemfanya Mourinho kuwatupia lawama wachezaji wake.

Licha ya Manchester United kupewa sapoti na mashabiki kwenye uwanja wake wa nyumbani, Arsenal ndio walianza kuzifumania nyavu za wapinzani wao kupitia kwa Shkodran Mustafi (26’) huku Anthony Martial akiisawazishia United (30’).

Alexandre Lacazette aliwainua mashabiki dakika ya 68’ huku bao hilo likidumu kwa dakika moja tu ambapo Jesse Lingard aliisawazishia Manchester United mnamo dakika ya 69’.

Matokeo mengine kwa mechi zilizopigwa jana usiku Burnley 1-3 Liverpool, Everton 1-1 Newcastle United, Fulham 1-1 Leicester City na Wolverhampton Wanderers 2-1 Chelsea FC

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW