Michezo

Mourinho kuwakabili Bayern Munich kimafia, kutua Allianz Arena na makinda ya Tottenham

Usiku wa leo, Jose Mourinho atakiongoza kikosi cha Tottenham kuwakabili Bayern Munich katika dimba la Allianz Arena mchezo wa Champions League huku inatarajiwa baadhi ya nyota wake muhimu kutokuwepo kwenye mechi hiyo akiwemo Harry Kane.

Tottenham team news predicted line up Bayern Munich

Kuna uwezekano Harry Kane na baadhi ya idadi kubwa ya wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza cha Tottenham kupumzishwa wakati vijana hao watokao Kaskazini mwa jiji la London watakapo ikabili Bayern Munich.

Hata hivyo timu zote tayari zimeshafuzu kuingia atua inayofuata ya michuano ya Champions League na kwa sasa Jose Mourinho anaweza kuwa na wakati wa kujaribu wachezaji wengine.

Mreno huyo tayari amekusudia kutomwanzisha Kane katika kikosi cha kwanza na baadhi ya wachezaji wengine.

“Matokeo haya jalishi, lakini ni muhimu kwa wachezaji, muhimu sana kwa wachezaji ambao wao ndiyo wanaokwenda kucheza.” Amesema Mourinho.

Jose Mourinho ameongeza kuwa “Sifahamu, ila siwezi kusema moja kwa moja kwamba Harry Kane hatocheza, lakini nani anakwenda kucheza nahitaji kulifikiria hilo.”

”Ni muhimu kwangu mimi kuwafahamu zaidi, hakika baadhi yao hawatocheza mechi hii tunayokwenda kucha.”

“Ni nafasi muhimu kwa wachezaji wachanga, ni muhimu kwao kwaajili ya kuwaendeleza, kama Walker-Peters, Troy Daniel Parrott, Sessegnons hawa wote ni nafasi yao.”

Wachezaji wengi makinda ambao huwenda watapewa nafasi kubwa hii leo ni pamoja na Troy Daniel Parrott mwenye miaka 17, Ryan Sessegnon miaka 19, Kyle Walker-Peters miaka 22, Oliver William Skipp miaka 19 na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents