Tia Kitu. Pata Vituuz!

Mourinho: Kwa mtazamo wangu, timu bora imeshindwa (Manchester United)

Pamoja na Real Madrid jana kuwafungashia virago Manchester United kwenye ligi ya mabingwa wa Ulaya na kuingia robo fainali, kocha wa Real Jose Mourinho, ameipongeza Man U kwa mchezo mzuri waliouonesha na kudai kuwa walistahili kushinda.

article-2288734-1876532B000005DC-524_634x428

Mourinho amesema kwa mtazamo wake timu bora ndio iliyoshindwa na kwamba kama Man wasingepata kadi nyekundu wangeshinda. Amesema refa wa mchezo huyo alipaswa kumpa kadi ya njano Luís Nani kwa kumchezea ndivyo sivyo Álvaro Arbeloa na sio kadi nyekundu.

11-25-02-558-163160571

Cristiano Ronaldo hakuionea huruma timu yake ya zamani baada ya kufunga goli lililoiwezesha Real Madrid kusonga mbele.

Alex Ferguson akilalamika baada ya Nani kupewa kadi nyekundu
Alex Ferguson akilalamika baada ya Nani kupewa kadi nyekundu

Magoli ya mawili ya Real Madrid yalifungwa na Luka Modric na Ronaldo baada ya United kuanza kuongoza kwa goli moja ambalo Sergio Ramos alijifunga. Kutokana na matokeo hayo, kocha wa United Alex Ferguson alikasirishwa na uamuzi wa refa Cuneyt Cakir kiasi cha kukataa kuongea waandishi wa habari na kumwachia msaidizi wake Mike.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW