Michezo

Mourinho: Liverpool ijiandae vilivyo siku ya Jumapili

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amewaambia mashabiki wake kwamba mechi ya Jumapili dhidi ya Liverpool haitakuwa ”matembezi ya ukumbi wa filamu’ na badala yake ameitaka Liverpool kujiandaa vilivyo.

Hatahivyo Mourinho amesema kuwa kila mchezaji anafaa kufanya kazi ya ziada dhidi ya Liverpool.

”Ni mechi muhimu sana kwetu, alisema.Tunapocheza vyema mashabiki pia hushirikiana nasi .

Tunaposhindwa kucheza vizuri ni vyema kwamba mashabiki hawapaswi kulalamika sana.

Kila mtu anapenda mechi kubwa, wachezaji,wakufunzi na mashabiki. Kila mmoja anapenda mechi kubwa kwa hivyo tuelekee katika mechi hiyo siku ya Jumapili”.

Liverpool imepoteza mara mbili pekee msimu huu ,ikiwa imeshindwa 4-3 na Bournemouth mnamo tarehe 4 mwezi Disemba.

Liverpool ni ya pili katika ligi ya Uingereza, ikiwa pointi tano mbele ya United iliopo katika nafasi ya sita na pointi tano nyuma ya viongozi wa ligi Chelsea.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents