Michezo

Mourinho: Lukaku na Ibrahimovic wakicheza pamoja ni moto wa kuotea mbali

Meneja wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anaamini kuwa washambuliaji wake Lukaku na Ibrahimovic kama wanacheza pamoja wanaweza kutengeneza umoja usiyo kamatika na kuisaidia timu hiyo kumaliza msimu katika kiwango bora.

Jose Mourinho amesema “Si hitaji kuwatengenezea mazingira kati ya Zlatan na Romelu kwa sababu inawezekana kwa upande wao, anaweza kuwa  Romelu na inawezekana asiwe yoyote kati yao.”

Mourinho anaamini wachezaji hao kama wanacheza pamoja wanaweza kuzalisha kitu muhimu sana mwisho wa msimu.

Mastraika hawa wawili kama watacheza pamoja inaaminika kuwa itaifanya United kuwa imara na yenye uwezo mkubwa na huwenda wakaifikisha katika kiwango kingine.

Nyota hao wa Manchester United hii leo watakuwa na kibarua mbele ya Watford Uwanja wa Vicarage Road katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza na tayari kikosi hicho kimeshawasili viunga vya Vicarage Road.

Msimamo wa Ligi ya Uingereza

Michezo ijayo inayo ikabili United

Kikosi cha Man United kikiwasili Watford

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents