Michezo

Mourinho: Man United hatubahatishi {Video+Picha}

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema kwamba haamini kwamba anacheza kamari kwa kuangazia zaidi ubingwa wa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League.


Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho.

Meneja huyo, ambaye ameamua kuangazia ligi hiyo baada ya kumaliza katika nafasi nne juu za Ligi ya Uingereza, anasema uamuzi wake ni wa busara.

https://youtu.be/fhKmJbJOwsU
Magoli ya timu zote mbili yalivyopatikana.

United wametinga hatua ya fainali ya michuano hiyo baada ya kutoka goli moja moja na klabu ya Celta Vigo hapo jana huku ushindi wa goli moja bila alioupata ugenini ukimbeba na kuhakikisha kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo.

United sasa itakutana na vijana wa Uholanzi, timu ya Ajax ambayo nayo imekata tiketi ya fainali baada ya ushindi wao dhidi ya klabu ya Lyon katika mchezo wa nusu fainali ya pili.


Goli la Mchezaji wa Manchester United,Marouane Fellaini.

“Ajax inayomuda wa kumpumzika maana ligi yao inaisha jumapili,” alisema Mourinho. “Wana nafasi ya siku 12 za maandalizi. Sisi tuna michezo mitatu na siku tatu.
‘Unitedi ina nafasi moja pekee’

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents