Michezo

Mourinho na Pogba washauriwa kuweka tofauti zao pembeni Manchester United

Mourinho na Pogba washauriwa kuweka tofauti zao pembeni Manchester United

Kiungo wa zamani wa klabu ya Manchester Unied Bryan Robson ameishauri bodi ya United ikijumuisha kocha wa timu hiyo Mreno Jose Mourinho kuziweka tofauti zao pembeni na kiungo Mfaransa Paul Pogba.

Robson amemshauri kocha huyo kufanya hivyo mara moja kwa lengo la kurudisha morali ya timu iliwaweza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali wanayoshiriki.

“Jose Mourinho na Paulo Pogba wanapaswa kuweka tofauti zao mbali na kushikamana ili kuipatia Manchester United matokea mazuri”  kufuatilia kile kinachosemekana wawili hao hawana maelewano, nahodha huyo wa zamani wa United  Bryan Robson ameiambia ESPN FC.

Licha ya Pogba kupewa nafasi ya nahodha wa mechi ya ufunguzi wa msimu dhidi ya Leicester, lakini kutokana na mgongano huo, alikataa kutoa nafasi ya kumaliza majadiliano ya furaha yake, akisema: “Kuna mambo na kuna vitu ambavyo siwezi kusema vinginevyo niyatapatie ufumbuzi ”

kutokana na hicho Robson anasisitiza ni muhimu kwa pande hizi mbili kuweka tofauti zao kwa upande mmoja na kuzingatia malengo ya timu.

“Ndani ya klabu ya mpira wa miguu unapaswa kupatana vizuri na kila mtu muwe pamoja, “Huna haja ya kuwa marafiki lakini, mnapokuwa katika timu moja mnatakiwa muwe kitu kimoja,na huu ndio wakati ambapo wote hutaa watu wote katika timu kuwa pamoja.”

Bryan Robson, Manchester United

Robson pia anaamini “wachezaji wa United wanahitaji kuchukua majukumu zaidi kwa kutafuta njia sahihi za kupata matokeo bora katika jitihada za kila mmoja  iwe kwa kupambana au kutiana moyo”

“Unahitaji kuwa na imani kutoka kwa wachezaji wako na wewe mwenyewe,” aliongeza. “Una budi kuanza kuinua mchezo wako mwenyewe”

“Sio kwamba wachezaji wote wanakuwa vizuru, lakini ni muhimu sana kuwahimiza wachezaji wako pia. Hilo ndio la msingi zaidi kwangu kwenye maisha ya mpira wa miguu ambapo, ukiwa kama kiongozi una jukumu katika chumba cha kuvaa uende kwa kila mmoja kuwahimiza kama unahisi kuna mchezaji kaonyesha uvivu au kaonyesha kuchoka mazoezini, Ikiwa kuna mmoja wao ana busara zaidi basi jaribu kumsikiliza na wengine wajifunze kutoka kwake”

Manchester United imekuwa na matokea mabaya katika mwanzo wa ligi hii katika michezo yake ya ufunguzi kwani imecheza michezo minne imeshinda michezo miwili na kupoteza michezo miwili hivyo inashikilia nafasi ya 10.

 

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents