Michezo

Mousa Dembele kutimka Tottenham Hotspur 

Kiungo wa klabu ya Tottenham, Mousa Dembele amezungumza na vyombo vya habari juu ya mustakabali wake ndani ya Spurs akiwa nchini Urusi kwenyemichuano ya kombe la Dunia.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, kandarasi yake na Spurs inatarajia kufikia tamati dirisha la usajili lijalo na hivyo bado hajahakikishiwa mkataba mpya ndani ya klabu hiyo huku akihusishwa kuelekea kwenye ligi ya China na Italia.

Alipoulizwa swali na vyombo vya habari nchini Urusi, Mbelgiji huyo amesema kuwa anaweza kutimka Tottenham na kamwe hatoweza kujiunga na klabu nyingine ndani ya ligi ya Uingereza huku kwa sasa akiwa anajaribu kuzungumza na marafiki zake wanao cheza nje ya nchi hiyo.

“Tottenham ni klabu yangu, familia yangu inajiskia furaha ikiwa hapa London na watoto wangu wanasoma shule hapa hivyo inakuwia ugumu kuondoka sehemu kama hii,” amesema Dembele.

“Nimeshazungumza na klabu za  China nimezungumza na Axel Witsel laikini pia nimezungumza na MLS na wengine wengi nikijaribu kujua hata habari kwa uchache tu. Itakuwa muda mzuri wa mimi kufanya chaguzi muhimu pakuelekea licha ya moyo wangu kutoridhia kuondoka ndani ya klabu ya Tottenham.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents