DStv Inogilee!

Movie Ya Zamora Yaonyeshwa Katika Tamasha La Filamu Za Ulaya

Movie ya Kitanzania iliyofanyiwa shooting Zanzibar ( Zamora) imekuwa filamu ya pekee ya kitanzania kwa mwaka huu kuonyershwa katika muendelezo wa Tamasha la filamu za Ulaya, utakaofanyika katika ukumbi wa viwanja vya ofisi za utamaduni wa Ufaransa ( Alliance Francaise ).
Filamu hiyo ya Zamora imetayarishwa na Shams Bhanji,ambaye ni mtayarishaji wa filamu mwenye asili ya kihindi na Uganda ambaye kwa sasa maskani yake jijini Zanzibar.Kivutio kikubwa Katika usiku washughuli ya uzinduzi huo wa filamu ilikuwa ni shoo kali kutoka kwa msanii Mafudh Mafudh wa Bendi ya Kipepeo kutoka Zanzibar ambaye anafanya muziki tofauti kabisa jinsi iliyozoeleka.
Msanii huyo ambaye anaimba mchanganyiko wa nyimbo za Neo Soul, Funk, R&B ambazo imechanganywa vionjo vya kiasili vya Sindimba, Kidumba na aina tofauti za ngoma za utamaduni akiwa amewashirikisha Mzee Kheri , mpiga ngoma, Christopher (gitaa la solo), Imani Obedi(Keyboard), Geofrey Derahai (electric drum) na yeye mwenyewe akipiga Accoustic gitaa.
Aidha katika onyesho la filamu ya Zamora na wahusika wake wakuu Richard Bendhouzeth, Richa Aidha na mwanadada Renalda Arbogast Ndaki ambao wameonyesha umahiri wao, na uwezo mkubwa wa kutumia viumbe asilia akitia for a katika vipande vyake kwa kumiliki Ngedere, kinyonga na nyoka na kuwafanya wahudhuriaji kuwa kwenye hali ya taharuki kira mara alipokuwa akionekana na wanyama hao.

Mtayarishaji wa muvi hiyo bwana Shams akiongea na mwakilishi wa Bongo5 .com alisema alitumia wiki mbili tu kufanya muvi hiyo na alitumia mandhari ya mji wa Zanzibar peke yake lakini aliamua kuwatumia washiriki kutoka Tanzania Bara ili kuweka na kuonyesha ladha tofauti na ile iliyozoeleka.
Akiendelea Bwana Shams anasema alitengeneza muvi hiyo akizingatia maisha halisi ya vijana wa Kizanzibari kwa kutumia mfumo wa utamaduni wa huko Tanzania Visiwani huku akiwaonyesha wapenzi wa Muvi za Tanzania namna Mapenzi yanavyoenda visiwani huko.
Angalia picha za usiku huo

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW