Burudani

Mpenzi mpya wa Amber Rose aendelea kuonyesha jeuri ya fedha

Mpenzi mpya wa membo Amber Rose, 21 Savage ameendelea kuonyesha jeuri ya kutumia fedha.

Rapper huyo mwenye miaka 24, amenunua cheni mpya yenye muonekano wa sura yake ikiwa imetengenezwa kwa madini ya almasi kwa kiasi cha dola 125,000 ambazo ni sawa na shilingi 279,856,507 kwa fedha za kitanzania ambapo kwa upande wa pili ina kinago cha Jason Voorhees.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, umesema Gabriel Jacobs ambaye ni mmiliki wa sonara ya Rafaello & Coiliyopo mjini Atlanta ambayo imetengeneza cheni hiyo, alitumia zaidi ya miezi miwili kuweza kuikamilisha.

Tukio hilo limetokea ikiwa ni wiki moja imepita tangu rapper huyo na mpenzi wake Amber walipomwaga kiasi cha fedha zaidi ya shilingi milioni 49 za kitanzania katika klabu ya usiku ya Club Crucial Jumatatu iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents