Soka saa 24!

 Mpiga picha amponza Koffi Olomide kuzuiwa kuingia Zambia

 Mpiga picha amponza Koffi Olomide kuzuiwa kuingia Zambia

Mwanamziki maarufu wa miondoko ya rhumba wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya  Congo (DRC), Koffi Olomide amekataliwa kuingia nchini Zambia kufuatia kuwa na makosa mengi yanayomkabili katika taifa hilo lililopo Kusini mwa Afrika na Ufaransa.

Olomide amezuiwa kuingia Zambia kutokana na uwepo wa madai ya kumshambulia mpiga picha katika hafla moja ya mziki alipokuwa ziarani nchini humo lakini pia uzalilishaji wa mnenguaji wake wa kike, kuwateka nyara pamoja na kuwalaghai katika ajira na kutumia vibali ghushi.

Kwa mujibu wa tovuti ya Lusaka Live Voice na Mwebantu za nchini humo zimeripoti kuwa Waziri wa nchi hiyo , Godfridah Sumaili amevitangazia vyombo vya habari kuwa Koffi Olomide atakamatwa endapo atakaidi na kufanya tamasha hilo aliloalikwa nchini Zambia.

Koffi Olomide ambaye majina yake kamili ni Antoine Christophe Agbepa Mumba alitarajiwa kufanya matamasha mawili nchini Zambia ambayo ni Julai 27  Lusaka na Mindolo Dam huko Kitwe Julai 28.

Siku ya Jumamosi balozi wa Ufaransa aliyopo nchini Zambia, Sylvain Berger ametishia kushirikisha maafisa usalama wa Interpol kumkamata Olomide aliyesema kuwa bado mashataka dhidi yake nchini Ufaransa hayajafutiliwa mbali.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW