Habari

Mpiganaji miereka anyongwa hadi kufa Iran

Iran imesema imetekeleza hukumu ya kifo dhidi ya mpiganaji miereka mmoja Navid Afkari hapo jana kwa kumuuwa mwanamume mmoja wakati wa maandamno dhidi ya serikali katika mwaka wa 2018 na kuibua shutuma kali na mshtuko kwa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa – IOC.

Mwendesha mashtaka mkuu wa mkoa Kazem Mosuavi, alinukuliwa katika luninga ya kitaifa akisema kuwa Afkari wa umri wa miaka 27 aliuliwa katika gereza moja katika mji wa Shiraz Kusini mwa nchi hiyo.

Idara ya mahakama ilisema kuwa Afkari alipatikana na hatia ya ”mauaji ya hiari” kwa kumdunga kisu Hossein Torkman, mnamo Agosti 2 mwaka 2018.

Kamati ya IOC imesema kuwa imeshtushwa na mauaji hayo na kwamba ”inakera mno” kwamba miito ya wanariadha kote duniani na mashirika ya kimataifa ilishindwa kuzuia hatua hiyo.

Iran executed wrestler whose case drew international attention - Insider

Katika ujumbe kupitia mtandao wa twitter, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alilaani hatua hiyo na kusema wanaishtumu vilivyo. Aliongeza kuwa ni shambulizi kali dhidi ya utu wa binadamu na kwamba sauti za raia wa Iran hazitanyamazishwa.

https://www.youtube.com/watch?v=IE21X8axCow

https://www.youtube.com/watch?v=W9wYja48ZCo

https://www.youtube.com/watch?v=FS9nYt9xkwA

https://www.youtube.com/watch?v=9VgAznN5r8k

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents