Burudani

Mpoto adondosha songi jipya.

Mrisho Mpoto amezindua wimbo mpya pamoja na video yake unaokwenda kwa jina la ‘Mama Siwema’  akishirikiana na Femina HIP na kampuni ya  D. Light  inayotengeneza na kusambaza taa zinazotumia nishati ya jua , wakiwa na lengo la kuhamasisha utumiaji wa taa za nishati ya jua.

Uzinduzi huo ulifanyika katika chuo cha kijerumani cha sanaa, Goethe,hivi karibuni na mgeni rasmi akiwa Gonche Materego ,Secretary General wa Tanzania arts. Materego alizindua halfa hiyo aliwashukuru FEMINA pamoja na baraza la sanaa  kwa kutumia sanaa kufanya kampeni ya  kuelimisha jamii jinsi ya kutumia taa za sola na kupata mwanga salama.

Gonche aliwataka wasanii waache kujikita kuimba mapenzi tu, na kubadilika, kuimba  nyimbo za kuleta mabadiliko ya kimaendeleo. alimpongeza sana Mpoto kwa kazi zake anazozifanya ni msanii jasiri anayeweza kusimama na kutetea jamii.

Awali Mpoto  ambaye ni balozi wa kampeni ya ”Haki ya mwanga Salama”alisema wimbo wa ‘Mama Siwema’ unaelezea hadithi ya Siwema, mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa na bidii ya hali ya juu masomoni, na kwa bahati mbaya alipoteza maisha yake kwa ajali ya moto wakati akijisomea kwa taa ya mafuta (chemli).

Mapemai Januari mwaka huu, Femina HIP na D.light kwa pamoja walizindua kampeni ya kitaifa ya Haki mwanga Salama, kwa lengo la kuchochea mabadiliko ili shule zote, wazazi na serikali watafakari na kuunga mkono matumizi ya taa za sola.

Zaidi ya yote niliguswa sana na janga la moto lililotokea katika shule ya bweni ya Idodi mwaka jana ,ambapo wanafunzi 12 walipoteza maisha kwa moto uliosababishwa na mishumaa.

‘Natumaini kwamba utachochea jamii kutafuta na kutumia nishati mbadala ambazo hivi sasa zinapatikana madukani ,na wanafunzi wakiwa wamepewa ofa maalum ya taa za kujisomea’ alisema Mpoto.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents