Mpoto kuwakilisha Afrika Ufaransa

Mpoto kuwakilisha Afrika Ufaransa
Msanii Mrisho Mpoto ataliwakilisha bara la afrika katika mashindano ya Ushairi yatakayofanyika nchini Ufaransa mwezi ujao

Mpoto alisema amepata bahati ya kushiriki
katika mashindano hayo yajulikanayo kama World Slum Championship
yatakayofanyika katika jiji la Ufaransa.

"Nathubutu kusema kuwa naiwakilisha Afrika katika mashindano hayo kwa
kuwa mimi ni mtu pekee niliyepata bahati ya kushiriki katika mashindano
hayo kutoka bara la Afrika" alisema.

Alisema mashindano hayo yatafunguliwa June 16 katika jiji la Ufaransa
na kuendelea kwa wiki nzima ambapo washairi mbalimbali watakuwa
wakichuana katika mashindano hayo.

Akiuzungumzia uzinduzi wa albamu yake iliyoingia sokoni mapema mwezi
huu, Mpoto alisema anataka kuufanya kabla hajaondoka nchini.

Albamu hiyo iliyoitwa jina la Salam zako Mjomba iliingia sokoni ikiwa
na jumla ya nyimbo tano ambazo ni Salam zako Mjomba, Nikipata Nauli,
Asanteni kwa Kuja, Poleni Wanangu na Mtu Huru.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents