Burudani

Mpunga wakusanywa kufariji wahanga wa mlipiko Uingereza

Baada ya kutokea mlipuko mwezi  Mei, nchini  Uingereza kupitia tamasha la Dangerous Woman la msanii, Ariana Grande, hatimaye kampeni ya Love Manchester wamefanikiwa kukusanya kiasi cha dola 324,000 kwa ajili ya waathirika wa tukio hilo.

Kwa mujibu wa ripoti iliyopo inaeleza kuwa kiasi cha dola milioni 24.5 zilitoka katika tamasha hilo lilioharibika na zaidi ya dola milioni 2 zilitoka kwa msanii huyo kupitia tamasha lake la ‘One Love liliofanyika mwezi Juni.

Gazeti la The Guardian la nchini humo lime ripoti kuwa familia zilizoathiriwa na tukio hilo wamepokea kisai cha dola 90,000 , kama mkono wa pole na wanatarajiwa kuongezewa kiasi kingine kabla ya mwisho wa wiki.

Tamasha la Dangerous Woman, lilitokea katika mjiji Manchester katika ukumbi wa Manchester Arena, na mlipuko ulisababisha vifo vya watu 22 na majeruhi zaidi ya 50 kuwa majeruhi.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents