Mr Blue amletea ‘mapozi’ msanii wa Kenya

Katika hali inayoonesha kuwa Mr. Blue aka Baba Sameer hajaacha mapozi, hivi karibuni amemwacha solemba msanii wa Kenya aliyesafiri hadi Tanzania kuja kufanya collabo naye.

Kwa mujibu wa meneja na mtu anayehusika na masuala ya marketing katika muziki nchini Kenya aliyejitaja kwa jina la Paul, msanii aitwaye Chika alimfuata kumwambia amtafutie msanii wa Tanzania watakayefanya naye collabo.

Paul ameiambia East Africa Radio leo kuwa alifanikiwa kupata mawasiliano na Mr Blue ambaye alimwambia ili afanye collabo waliwatakiwa kumlipa shilingi laki moja pamoja na nauli ya taxi ya kwenda na kurudi kwenye studio ya AM Records.

Alisema walimlipa fedha hizo na kweli alienda kuingiza sauti zake ambazo hata hivyo kwa mujibu wa producer ambaye ni mdogo wake Manecky, sauti zake zilikaa vibaya kwenye beat hivyo alitakiwa kwenda kurudia.

Paul amesema Mr Blue alikataa kwenda kufanya sauti zingine labda kama wangemlipa tena kiasi kama cha mwanzo.

Hata hivyo meneja huyo amesema haiwezekani walimpe kiasi kingine cha fedha wakati kazi aliyotakiwa kuifanya haikukamilika.

Alimuomba Kabayser ambaye kwa sasa yupo nchini India kufanya kazi hiyo kwakuwa imewagharimu kiasi kikubwa cha fedha kuja mara kadhaa nchini kwaajili ya kufuatilia sauti hizo na kwamba soko la Afrika Mashariki ni dogo hivyo ni muhimu wakisaidiana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents