Mr. Chuzi aingia kwenye usambazaji wa filamu

Tuesday-KIhangara-cut

Muigizaji na muongozaji wa filamu nchini Tuesday Kihangala aka Mr. Chuzi, ameamua kuingia pia kwenye shughuli za usambazaji wa filamu.

Mr. Chuzi atakuwa akifanya kazi hizo chini ya kampuni yake ya Tuesday Entertainment.

Kwa kuanza tayari Chuzi ameshafanya mazungumzo na waigizaji wakubwa watatu wa kike ili kuanza kusambaza kazi zao.

Wakati huo huo, Chuzi anatarajia kuingiza sokoni mwezi January, 2013 tamthilia mpya iitwayo High Heels ambayo inajumuisha waigizaji wengi wa Jumba la Dhahabu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents