DStv Inogilee!

Mr. Ebbo afariki

mr_ebbo

Msanii wa kizazi kipya, Abel Motika anayejulikana kama Mr.Ebbo jana usiku aliaga dunia baada ya kusumbuliwa maradhi kwa muda mrefu.

 

Chanzo hasa cha kifo chake hakijajulikana mpaka sasa lakini taarifa zinasema mipango ya kuusafirisha mwili wa marehemu unafanyika kurudisha nyumbani kwao Arusha tayari kwa mazishi.

Msanii huyo ambaye ameacha pengo kubwa kwenye sanaa ya muziki Tanzania atakumbukwa zaidi kwa kudumisha mila yake ya kimasai kwa mavazi, lafudhi na vilevile kimuziki.

Tutazidi kukuhabarisha muendelezo wa habari hii.

Mungu ametoa na Mungu ametwaa, jina la bwana lihimidiwe milele

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW