Habari

Mr Nice alia!

NiceLucas Mkenda/Mr Nice akiwa nchini Uganda alikoenda kutimiza mualiko wa shoo moja lakini inasemekana amekula vimeo vya shoo ishirini zaidi, ameamua kulia na vyombo vya habari vya hapa bongo.

Mr NiceLucas Mkenda/Mr Nice akiwa nchini Uganda alikoenda kutimiza mualiko wa shoo moja lakini inasemekana amekula vimeo vya shoo ishirini zaidi, ameamua kulia na vyombo vya habari vya hapa bongo.

 

Na haya ndio maneno yake mwenyewe mfalme:

 

“Nasikia kuna gazeti limenisema vibaya huko home, eti! Sijui kiingereza na nashindwa kuongea na wazungu huku Uganda… Jamani! Naenda Amerika, Uingereza, Japan, Ujerumani na kwingineko kila kukicha, je! Huko natumia lugha gani? Kichaga au?”

 

“Nimegundua kuwa kuna baadhi ya watu wameanzisha mtaji wa kunisema vibaya kwa kuwa wanajua watauza kwa wingi hasa kwa mashabiki wangu.”

 

“Ama kweli nimeamini mti wenye maembe matamu ndio unaotupiwa mawe zaidi, ninachoomba wasisahau kuwa mazuri ni mengi nifanyayo pia kama kuwasaidia mayatima n.k. nayo wawe wanaadika.”

 

“Tukubaliane kuwaMr Nice ninapokuwa nje ya nchi siwi kama Mr Nice bali kama bendera ya Tanzania na hii si kwangu tu bali kwa wasanii wote, kwa hiyo kumponda msanii badala ya kumsapoti ni sawa na kuponda bendera yako.”

 

“Kama unataka kuandika habari kuhusu msanii usikurupuke tu kwa sababu una kalamu na karatasi! Kwanza najua Kiswahili ni lugha ya kimataifa, mimi sikuja kutafuta wazungu huku nilipo maana hata hapo bongo wamerundikana kibao tena wanamjua Mr Nice vizuri zaidi.”

 

“Mimi nipo Kampala kimuziki na naheshimiwa kama mwamba kutoka TZ, ni sifa kwetu sote wala si peke yangu kama Mr Nice, kama mwaniandika sijui kingeli ni sawa, ila msisahau kuwa Kiswahili ndicho kinachonizungusha duniani kila siku na nikifika huko vile vile hutumbuiza kwa Kiswahili pia, nadhani nahitaji sapoti kwa wanahabari wote bila kujali kabila, dini wala jinsia.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents