Burudani

Mr. Nice apongeza kufungiwa nyimbo za wasanii zisizo na maadili

Mwanamuziki Mr. Nice ameipongeza serikali kwa hatua iliyochukua ya kuzifungia nyimbo za wasanii zisizo na maadili.

Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Tuheshimiane’ ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa hatua hiyo ni sawa kwa sababu nyimbo hizo zitaharibu vijana na watoto ambao ndio wafutialiaji wakubwa wa muziki.

“Unajua vijana, watoto wadogo ndio wanapenda zaidi muziki sasa hivi, mimi kama msanii nikiimba kitu ambacho hakina maana, mantiki, adabu ni vibaya,” amesema.

“Serikali inaona ni ajira yako lakini isifike maali ukachafua watu wengine, ni afadhali wewe samaki mmoja ukatupwa wengine waendelee kuchanua, sio wote waonekana wameoza,” amesisitiza.

Soma Zaidi; TCRA yazifungia nyimbo 15, Diamond na Nay maumivu zaidi

Wiki iliyopita Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilipokea list ya nyimbo 15 zisizokuwa na maadili kutoka kwa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) na nyimbo hizo kufungiwa. Miongoni mwa wasanii nyimbo zao zilizofungiwa ni Diamond, Nay wa Mitego, Snura na Roma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents