Mr Nice awa dhahabu Kenya, asainishwa label moja na DNA, kuhamia huko, atafanya tour nchi nzima

By  | 

Radio, blogs/website na vyombo vingine vya habari nchini Kenya jana vilitawaliwa na habari za Mr. Nice ambaye inasemekana ameamua kuhamia nchini humo.

Mr Nice akiongea na waandishi wa habari

Mr Nice akiongea na waandishi wa habari

Jana hiyo hiyo ametoa video ya wimbo aliofanya na DNA, Tafuta. Akiwa nchini humo Mr Nice alidai kuwa ana mpango wa kufanya show nchi nzima ambako ana mashabiki wengi kuliko Tanzania ambako anaonekana amefulia.

Familia mpya, maisha mapya

Familia mpya, maisha mapya

Wakimsikiliza Nice

Wakimsikiliza Nice

Katika mahojiano, Mr Nice alidai kuwa ni wakenya ndio waliomnunulia gari lake la kwanza na hivyo anahisi wanamdai. Tayari amesainishwa kwenye lebel ya Grandpa Records ambako atakuwa pamoja na wasanii wengine wa label hiyo wakiwemo Kendi, DNA, na Dashy Crew!

mr_nice_4

Tarehe 26 mwezi huu atapiga show yake ya kwanza kwenye ukumbi wa Florida 2000, tarehe 27 atapiga show kwenye uwanja wa Nyayo kwenye Kids Festival. Anatarajia kutoa albam yake ya sita mwezi June na itaitwa Chali Wa Kibera, ambapo wimbo wenye jina hilo pia utatoka hivi karibuni.

Mr Nice akipata treatment ya VIP nchini Kenya

Mr Nice akipata treatment ya VIP nchini Kenya

Staa huyo wa Kidalipo aliongea na waandishi wa habari waliomuuliza maswali mengi ambayo inasemekana aliyajibu kwa ufasaha mkubwa.

mr_nice_7

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments