Burudani

Mr Nice azushiwa kifo kwenye mitandao ya kijamii

Msanii mkongwe wa muziki, Mr Nice amesikitishwa na watu ambao wamemzushia kifo katika mtandao wa kijamii.

Mtandao mmoja wa kijamii uliandika taarifa za uongo kwamba muimbaji huyo amefariki akiwa nchini Tanzania.

Mr Nice ambaye yupo nchini Kenya amesema alishangaa kuona watu wakimpigiwa simu kwa nyingi na kuulizwa kuhusu afya yake na alivyofuatilia akagundua kuna mtandao umeandika taarifa za uongo kwamba amefariki.

Kupitia facebook, Mr Nice aliamua kuandika taarifa hii:

East africa vibes nawashukuruni sana kwa kunizushia kifo sina la kuwajibu ,,ila mungu awalipe kadri ya vile mnavyostaili kwa hiki mlichonizushia leo ….mungu ni wetu sote na hasikilizi amri za binadamu so atakaponihitaji ataniita kwa mapenzi yake but si nyie east african vibes mnaoweza kuniua wala yeyote yule chini ya hili jua …kama nyie hamuioni thamani yangu hilo ni juu yenu kwani huku niliko mimi ni kama lulu na maisha yanaendelea tena kwa kiwango cha juu kabisa ..hii si mara ya kwanza kunizushia kifo na mambo mengine ya ajabu ajabu ila all in all mi nipo na bado mtaniona sana nikiendelea kuwepo ….im total dissapointed kwakweli …mungu awape stahiki yenu ..THANKS SANA EATV 13/12/2016

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents